Wiki ya Huduma za Fedha

Kutoka kushoto aliyekaa Mhe. Jamal Kassim Ali, Waziri wa Fedha Zanzibar Kwenye Picha ya Pamoja na Viongozi Pamoja na Wawakili wa Taasisi Mbali Mbali ikiwemo PBZ BANK.

Benki ya Watu wa Zanibar (PBZ BANK) tumepata fursa ya kushiriki Wiki ya Huduma za Fedha inayo adhimishwa kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dareslaam ambayo imelenga kuwaelimisha Watanzania kuhusu masuala ya kifedha kwa lengo lakuwajengea uwelewa juu yanamna yakutafuta fedha, kuitunza, kuiendeleza, pamoja na kujiandaa kwa maisha ya uzeeni au maisha baada ya kustaafu.

Maadhimisho hayo yamefunguliwa rasmi tarehe 10/11/2021 na Mhe. Jamal Kassim Ali, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Picha ya Pamoja kati ya Wafanyakazi wa PBZ BANK na Baazi ya Wateja.

Pamoja na mambo mengi mazuri yanayofanywa na PBZ BANK viwanjani ikiwemo utowaji wa elimu juu ya masuala ya kifedha pia zinapatikana huduma za; ufunguwaji wa account, fursa za mikopo, kupokea maoni ya wateja pamoja na kuwatatulia changamoto zao zinazohusiana na huduma zetu.

Mafunzo kwa Wastaafu Watarajiwa PBZ PREMIER LEAGUE