UDHAMINI WA MASHINDANO YA QURAAN

Mshiriki wa Mashindano ya Quraan Akisoma Quraan

PBZ IKHLAS tulipata fursa ya kuyadhamini Mashindano Makubwa ya Qur’aan Afrika yaliyofanyika tarehe 17/04/2022 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kaitika jiji la Dareslaam, nchini Tanzania. Mashindano hayo yaliwashirikisha washiriki kutoka nchi mbali mbali za kiafrika ikiwemo Tanzania.

Mhe. Mgeni Rasmi, Dr. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar, akifuatilia kwa Umakini Mashindano

Mashindano haya kwa usimamizi wa taasisi ya Alhikma Foundation Tanzania, hufanyika kila mwaka, lengo pamoja na malengo mengine mengi mazuri, pia kuwashajihisha vijana wa kiislam kuipenda Quráan sambamba na kujiweka karibu na Mungu.

Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ BANK Dr. Muhsin Salim Masoud Akitoa Nasaha Zake

Kupitia hadhara hiyo Dr. Muhsin ametowa shukuran zake za dhati kwa ya PBZ kwa Mhe. Rais kwa kukubali kujumuika na Watanzania katika kufanikisha shuhuli hiyo, pia kuwashukuru Alhikma Foundation kwa kuandaa na kusimamia mashindano hayo, ambapo pia ametumia fursa hiyo kuwaahidi waislam na watanzania kwa kujumla kuwa PBZ itaendelea kutowa ushirikiano kwa shuhuli hiyo na nyengine nchini.

Mshindi wa Kwanza Akikabidhiwa Zawadi Yake ya 20,000,000/=
Mshindi wa Pili Akikabidhiwa Zawadi Yake
Mshindi wa Tatu Akikabidhiwa Zawadi
Mshindi wa Nne Akipokea Zawadi Yake
Mshindi wa Tano Akikabidhiwa Zawadi Yake

NEW CHARGES AND FEES FOR BANK PRODUCT AND SERVICES - 2022 MAFUNZO YA ZAKAH