PBZ BANK TANDAHIMBA

Tawi jipya la PBZ BANK TANDAHIMBA

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ BANK) katika kuhakikisha inaunga mkono juhudi za Viongozi wetu wakuu wa Nchi, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kutekeleza sera jumuishi za masuala ya kiuchumi kwa wananchi, imewasogezea wananchi wa Tandahimba huduma za kifedha karibu yao kwa kufungua tawi jipya wilayani hapo (PBZ BANK TANDAHIMBA).

PBZ BANK, katika kuboresha na kutanuwa huduma zake, marakwamara hubuni mikakati imara ikiwemo hii yakufunguwa matawi mapya maeneoneo tofautitofauti, pamoja na malengo mengine mengi mazuri, pia kuwaondolea usumbufu wananchi katika kuzifata huduma za kifedha umbali mrefu.

MAFUNZO YA ZAKAH Mafunzo kwa Wastaafu Watarajiwa