Mkutano wa PBZ BANK na PBZ MAWAKALA

Picha ya Pamoja kati timu ya Pbz ikiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Pbz wa katikati kati ya waliokaa, Dr. Muhsin Salim Masoud na baazi ya Mawakal.

Siku ya Jumamosi tarehe 18/09/2021, tumekutana na Mawakala Wetu(PBZ WAKALA) katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil, visiwani Zanzibar kwa lengo la kuwapatia mafunzo pamoja na kupokea changamoto wanazokutana nazo katika kutowa huduma. Hii yote ni kwadhumuni la kuboresha huduma za Uwakala ambapo huduma hizi kwa sasa zimekuwa muhimu mno kwetu sisi kama benki lakini pia na kwawananchi.

Mkurugenzi Mwendshaji Pbz akibadilishana mawazo na baazi ya Mawakala

Kupitia mkutano huo Dr. Muhusin Salim Masoud amesema Pbz itaongeza juhudi zakusambaza Mawakala wa Pbz nchi nzima (Tanzania Bara na Visiwani) ili kuwawezesha wananchi kuweza kupata baazi ya huduma za kifedha pasina ulazima wakufika benki. Malengo yake nikuona siku moja kila mtaa una Pbz Wakala.

Picha ya Pamoja Kati ya Timu ya Pbz na Pbz Mawakala

PBZ WAKALA ni rahisi, salama, nafuu na inaokoa muda. Karibu kwa PBZ WAKALA aliyekaribu yako akuhudumie.

Malipo ya SMZ kupitia Ushirikiano wa PBZ na Tigo Pesa Mashindano ya Ligi za Kitaasisi