Mikutano ya YUNA, Iliyofanyika Zanzibar.

Picha Meza Kuu Ikiongozwa na Mgeni Rasmi (Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi)

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ BANK), tarehe 23/08/2021 tulipata fursa ya kushiriki ufunguzi wa mikutano ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Kimataifa(YUNA – Youth of the United Nations Association) iliyofanyika visiwani Zanzibar, yenyelengo la kuwajenga vijana kwakuwapa fursa za kujadili kwa pamoja masuala mbali mbali ya kilimwengu ikiwemo Maendeleo Endelevu ( Elimu, Afya, Ajira na Amani)

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi akitowa nasaha zake kwa vijana wa kimataifa kupitia jukwa hilo. Pia Mhe. Kitwana amepata fursa ya kuwakaribisha wadau mbali mbali kuchangamkia fursa ambazo zinapatikana kupitia uchumi wa bluu (Blue Economy) visiwni humo, ambalo nieneo la kimkakati linalotiliwa nguvu na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi wa Rais Dr. Hussein Ali Mwinyi .

Mshiriki Kutoka Ubalozi wa Ujerumani Nchini Tanzania

Mwakilishi wa Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzinia naye alipata fursa ya kutowa nasaha zake kwa vijana, ambapo pamoja na mambo mengine amewataka vijana kufata nyenendo njema ikiwemo kujifunza kila siku mambo tofautu tofauti mazuri kwani wao ni viongozi wa kesho.

Washiri, Vijana Kutoka Mataifa Mbali Mbali

Mikutano ya namna hii hufanyika kila mwaka nchi tofauti tofauti, mwaka huu 2021 ni zamu ya Tanzania nahivyo imefanyika Zanzibar kama sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Vijana wa Kitanzania nao kama sehemu ya vijana hao, walipata fursa yakushiriki na kujadiliana na vijana wenziwao wa mataifa mengine mambo tofauti tofauti yakilimwengu.

Wakwanza Kutoka Kushoto ni Mwakilishi Kutoka Pbz

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ BANK), ni desturi yake kushirikiana na jamii katika kujenga hatima njema za jamii husika, eidha zile za hapa nchini au hata zile za kimataifa, lengo nikujenga mahusiano chanya kati ya benki na jamii lakini pia kujenga kwapamoja ustawi mwema wa kijamii.

Picha ya Pamoja Miongoni Mwa Washiriki na Mgeni Rasmi

Dunia yenye watu wenye Afya, Amani na Ustawi bora inawezekna, kwapamoja tushirikiane kuijenga dunia yetu.

Mashindano ya Ligi za Kitaasisi Pbz na Udhamini wa Yamle Yamle Cup