Mafunzo kwa Wastaafu Watarajiwa

Afisa Uhusiano wa PBZ BANK, Ndugu Salim Hassan Iddi, Akitowa Mafunzo kwa Wastaafu Watarajiwa

Siku ya Alhamis tarehe 25/11/2021 Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ BANK) kwa kushirikiana na Zanzibar Social Security Fund (ZSSF), pamoja na wadau wengine katika Ukumbi wa Michenzani Mall, Zanzibar, tumepata fursa ya kutowa Elimu kuhusu masuala ya kifedha kwa Wastaafu watarajiwa. Elimu hiyo imelenga katika kuwaongoza Wastaafu hao watarajiwa katika kuchaguwa ni mambo gani mazuri ya kuyaendea na mambo gani mabaya yakujiepusha nayo mara tu baada yakustaafu na kupewa kiiunuwa mgogo pamoja na pensheni.

Wastaafu Watarajiwa Wakifatilia Mafunzo kwa Umakini Mkubwa

PBZ tunayo account maalumu kwa ajili ya Wastaafu (STARA ACCOUNT) ambayo haina gharama ya kufungulia wala makato ya mwisho wa mwezi, kizuri zaidi kupitia account hii mstaafu anaweza kupata mkopo mzuri (STARA LOAN), karibu sana. Mstaafu ili kufunguliwa account hii anatakiwa kutembelea tawi letu lililokaribu nae akiwa na kopi ya kitambulisho kati ya Mzanzibari Mkaazi, NIDA, Leseni ya udereva au Passport ya kusafiria na picha mbili za passport size. Account hii haina gharama za kufungulia wala makato ya mwisho wa mwezi.

Wastaafu Watarajiwa Wakiendelea Kufatilia Mafunzo kwa Ukaribu Zaidi.

PBZ BANK mara kwa mara imekuwa ikijitowa vilivyo katika kuisaudia jamii kupitia nyanja tofauti tofauti lengo kubwa likiwa nikuwaunga mkono viongozi wetu wa nchi katika kuleta ustawi bora kwa mwananchi mmoja mmoja, jamii na Taifa kwaujumla.

Mama Zetu Nao ni Wehehemu ya Wastaafu Watarajiwa Walio Faidika na Mafunzo Hayo

PBZ BANK TANDAHIMBA Wiki ya Huduma za Fedha