Customer Service Week

Mkurugenzi Mwendeshaji Pbz Dr. Muhsin Salim Masoud na baazi ya wateja wetu wakikata keki

Customer Service Week (Wiki ya Huduma kwa Wateja), Mkurugenzi Mwendeshaji Dr. Muhsin Salim Masoud, ameshiriki sherehe za Customer Service Week kupitia matawi yetu yalioko Mtwara, ambapo pamoja na mambo mengine, pia alipata wasaa wakufurahi na wafanyakazi pamoja na wateja kwaujumla.

Picha yapamoja kati ya Dr. Muhsin Salim Masoud (aliyesimama mwazno kutoka kushoto) na wafanyakazi.

Pia Dr. Muhsin Salim Masoud alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha Watanzania wote ambao hawajajiunga na PBZ ,kuitumia fursa hiyo kujiunga kwasababu Benki inatowa huduma bora kwa gharama nafuu na kwawakati muwafaka.

Wafanyakazi wa PBZ MTWARA Wakilishana Keki Katika Sherehe Hizo.

Wakati huohuo Mkurugenzi Mwendeshaji kupitia sherehe hizo ameutanabaisha Umma kuwa Pbz inamkakati mkubwa wakutaka kuongeza nguvu Tanzania Bara ikiwa nipamoja na kuongeza Matawi ya Pbz, ambapo ametowa mfano hai kuwa, hivi karibuni Benki itafunguwa matawi yake mawili Makao Makuu ya Nchi, Dodoma.

SUZA ORIENTATION WEEK Mjadala wa Fursa za Kiuwekezaji Zanzibar